• NEWS & SPORTS

    TANZANIA MPYA

    Tuesday, August 19, 2014

    DIAMOND HII SASA IMEZIDI




    Mkali wa Bongo fleva,Nasibu Abdul ‘Diamond’.



    Nasibu Abdul ‘Diamond’. Bila shaka u-mzima wa afya na unaendelea na michakato yako ya kujiingizia kipato. Binafsi mimi pia ni mzima wa afya na ninaendelea na mihangaiko yangu ya kila siku. Leo nimekukumbuka kwa mara nyingine kupitia barua kutokana na mwenendo mzima wa maisha yako, hususan maisha ya kimapenzi. Yawezekana ukaona kama nakushambulia lakini kimsingi lazima nikwambie ukweli kwa kuwa wewe ni kioo cha jamii. Kama unavyojua, muziki wako unakubalika. Hilo halina ubishi, hata mimi mwenyewe ni shabiki wako mzuri, nafuatilia sana kazi zako, lakini kitendo chako cha kucheza na hisia za wanawake hakileti picha nzuri katika jamii inayokuzunguka, achilia mbali mashabiki wako wanaokufuatilia. Takwimu inaonesha umekuwa na ‘trend’ ya kubadilibadili wanawake. Kinachonichosha zaidi ni pale unapoanzisha uhusiano na mwanamke na kisha kuachana naye kwa maneno ambayo hayaleti picha nzuri kwa mtu ambaye ‘mlishea’ naye vitu vingi katika uhusiano wenu. Mbaya zaidi maneno hayo yanapokuwa ya udhalilishaji. Kwa nini umdhalilishe mwanamke eti kwa kuwa humhitaji kwa wakati huo? Siyo sawa hata kidogo, ni bora ukaishi na mtu hata kama mtafikia hatua ya kuachana, basi muachane kwa kheri. Kipindi flani uliwahi kuwa na uhusiano na mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’, ukadaiwa kumrekodi sauti aliyekuwa mpenzi wako Wema Sepetu ambayo alikuwa akikuomba msamaha, ukairusha katika mitandao mbalimbali ya kijamii kitu ambacho hakikuwa sawa. Kama hiyo haitoshi, baada ya kumwagana na Penny na kurudiana na Wema, juzikati tena nimesikia umemshushia maneno mpenzi wako huyo wa sasa kupitia mtandao wa Instagram. Umeonesha kwamba wewe uko sahihi kutokana na mafanikio uliyoyapata na kuwataka watu wamshauri mpenzi wako apunguze starehe na maneno mengine yenye sura ya kumdhalilisha. Kwa kitendo chako cha kuandika vile, kinaonesha dhahiri kabisa maneno yale yalikuwa na walakini. Yanaonesha udhalilishaji. Huwezi kumwambia mtu unayempenda ashauriwe na watu wengine. Yakupasa wewe umshauri kwa lugha nzuri na si kumnadi mitandaon


    Tena mtu huyohuyo ndiye ambaye wiki kadhaa zilizopita ulimtolea kauli ‘tata’ ya kumwambia hutamuoa. Unategemea nini? Akueleweje? Wema huyohuyo ndiye ambaye umemtumia katika moja ya shoo zako hivi karibuni na kufanya mashabiki wafurahie, kweli anastahili kuambiwa maneno hayo? Kwa kulitambua hilo, nikushauri ubadilike kwa kila kitu unachotaka kumtendea mwandani wako, kauli kama hizo zinaweza kuwa sumu mbaya ambayo itakusumbua hata kama ukiwa na mafanikio kiasi gani. Waswahili wanasema mambo ya ndani yanabaki kuwa ya ndani, unapoona mwenzako anakosea, mweke chini mkiwa wawili umwambie. Hata kama hamtafikia muafaka mkiwa wawili, wapo wazazi ambao mnaweza kuwashirikisha na kusuluhisha matatizo yenu

    No comments: