Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Alexander Mnyeti ameagiza kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa ITV wa mkoani Arusha, Khalfan Liundi kwa tuhuma za kuandika habari za uchochezi.
Kukamatwa huko kwa Liundi kumekuja siku chache baada ya kufanya mahojiano na wananchi waliokuwa na malalamiko ya maji wakidai maji yamefungwa kwa siku saba.
Wafanyakazi wenzake ambao ni pamoja na mpigapicha wake walielezea tukio hilo la kukamatwa kwa mwandishi huyo ambapo walisema kuwa Askari walifika katika ofisi zao na kusema kuwa walikuwa wanahitajika kituo cha Polisi kwa ajili ya mahojiano. Walipofika waliabiwa kuwa wanahitajika kwa Mkuu wa Wilaya na baada ya hapo ndipo mwandishi huyo akakamatwa.
Hapa chini ni video ya mashuhuda wa kukamatwa kwa mwandishi huyo wa ITV
p;
No comments:
Post a Comment