• NEWS & SPORTS

    TANZANIA MPYA

    Thursday, September 11, 2014

    Sitta:NITAKOMAA NA BUNGE LA KATIBA HADI TAREHE 4 OCTOBA

    Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta ‘amekomaa’ kuhakikisha Bunge Maalumu la Katiba linafanya kazi kwa kasi na kukamilisha kila kitu ifikapo tarehe yake ya mwisho, Oktoba 4, ikiwamo kupiga kura za kupitisha Katiba inayopendekezwa kazi ambayo amesema itafanywa hadi nje ya nchi kwa wajumbe watakaokuwa huko. Sitta alilazimika kutoa matamko mawili kwa nyakati tofauti, mara ya kwanza wakati kikao cha Bunge kilipoanza jana akieleza jinsi Rasimu ya Katiba inayopendekezwa itakavyokamilika ifikapo Septemba 21 na baadaye mchana wakati akiahirisha Bunge alipotangaza mikakati ya kukusanya kura za wajumbe hadi nje ya nchi kuanzia Septemba 26, mwaka huu. Sitta alitumia fursa hiyo kuwataka wajumbe wa Bunge hilo watakaokuwa nje ya nchi kwa matibabu au sababu nyingine kuacha mawasiliano yao ili waweze kupiga kura wakiwa hukohuko. Alisema uongozi wa Bunge umeanza kufanya mawasiliano na balozi mbalimbali za Tanzania nje ya nchi ili wawepo watumishi wake watakaokula kiapo cha kisheria iliwasimamie upigaji kura.


    sitta

    No comments: