Sherehe
za Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanzania Bara zitakuwa zikifanyika
mjini Dodoma kuanzia mwaka 2017 badala ya Jijini Dar es Salaam kama
ilivyozoeleka.
Uamuzi
huo umetangazwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri
Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. John Magufuli, wakati
akitoa salamu zake za maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara,
kwenye sherehe zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru dar es Salaam.
Katika
salamu hizo, Rais Magufuli ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi, ameeleza
sababu za kufuta sherehe hizo mwaka jana na kuruhusu mwaka huu
zifanyike ambapo amesema sababu moja wapo iliyomfanya afute sherehe hizo
mwaka jana ni kubana matumizi.
"Mwaka
jana nilipouliza gharama za sherehe zile nikaambiwa ni shilingi bilioni
4, nikashangaa, bilioni 4 zote ni za nini?" Amesema Rais Magufuli.
Kuhusu
sababu za kuruhusu mwaka huu sherehe hizo zifanyike, Rais Magufuli
ametaja sababu mbili ambazo ni pamoja na kutumia gharama ndogo huku
sababu ya pili akiitaja kuwa ni kutokana na kwamba hizi ni sherehe za
mwisho za Uhuru kufanyika Jijini Dar es Salaam huku akieleza kuwa
kuanzia mwaka 2017, sherehe hizo zitakuwa zikifanyika katika makao makuu
ya nchi Dodoma.
"Mwaka huu gharama ni ndogo, hata kula wala kunywa hakuna, baada ya hapa hakuna kula wala kunywa"
Rais
Magufuli pia ametumia nafasi hiyo kuelezea mafanikio ya Tanzania katika
miaka yake 55 ya Uhuru, huku akieleza mikakati ya serikali yake ya
awamu ya tano katika kuifikisha nchi kwenye kipato cha kati na
kuwashukuru viongozi wakuu wa awamu zilizopita.
Kaulimbiu
ya sherehe hizo kwa mwaka huu ni: Tuunge mkono jitihada za kupinga
rushwa na ufisadi na tuimarishe uchumi wa viwanda kwa maendeleo yetu.
No comments:
Post a Comment