Msanii wa Nigeria ambaye amekuwa akifanya vizuri kwa mwaka 2016 Wizkid,
usiku wa December 8 kuamkia December 9 2016 ameingia kwenye headlines,
baada ya kuamua kukubali ushauri wa daktari wake wa kupumzika na
kusogeza mbele ratiba ya show zake.
Wizkid
kupitia account yake ya instagram ameamua kuwaeleza washabiki wake
kuhusu ushauri aliyopewa na daktari wake, baada ya kufanya show nyingi
bila kupata muda wa kutosha kupumzika, Wizkid ameandika maneno 118 kuomba radhi mashabiki wake baada ya kuamua kupumzika kufanya show.
“Team
Wizkid nimekuwa nikisafiri mfululizo kwa kipindi cha miaka miwili
kufanya kitu ninachokipenda bila kupumzika, nachukia uamuzi huu lakini
daktari wangu ameniambia niahirishe show zangu za mwaka huu na mwezi
January 2017 ili nipumzike”
“Naomba radhi mashabiki
wangu wote duniani hususani wa Nigeria na Uganda, nawaahidi kurudi
nikiwa vizuri na nikiwa na afya njema, nawaahidi kuwaletea muziki mzuri
kabla ya mwaka huu kuisha, niwatakie sikukuu njema ya Christimas na
mwaka mpya”
No comments:
Post a Comment