Kiungo na mkongwe wa zamani wa Arsenal Patrick Vieira ameweka wazi mtazamo wake kuhusu mwenendo wa Man United na Jose Mourinho wa kutopata matokeo mazuri, Vieira amewahi kufundishwa na kufanya kazi na Jose Mourinho kati ya mwaka 2008/10 wakiwa Inter Milan.
“Sijui
kama amepoteza mbinu zake na sifikiriii kama amebadili falsafa au mbinu
zake, nafikiri amekuwa akiendelea na utaratibu wake wa kupambana siku
zote kama kawaida, huenda ni mapokeo ya wachezaji unajua kizazi cha soka
cha sasa hivi kimebadilika kabisa”
“wakati tupo Inter kila kitu
kilikuwa kinaenda sawa na mapokeo yalikuwa mazuri na kwa haraka sasa
hivi kizazi kimebadilika, nahisi kuna wachezaji ambao inawezekana wakawa
hawamuogopi na wanaweza kusimama na kuongea chochote kitu ambacho
nahisi kinafanya mambo kuwa magumu zaidi”
No comments:
Post a Comment