Maamuzi hayo ni sehemu ya maazimio manne
ya Bunge yaliyopishwa usiku huu dhidi ya viongo wanaoteuliwa na Rais
hasa wakuu wa mikoa na wilaya, ambapo azimio lingine ni kumtaka Waziri
wa TAMISEMI kutoa maelekezo kw wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kufanya
kazi kwa mujibu wa sheria na kutoingilia majukumu yasiyo yao.
Hatua hiyo inafuatia hoja iliyotolewa
bungeni hapo na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, kufuatia kauli
inayodaiwa kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda
inayodaiwa kuwa ni dharau kwa Bunge.
Pia Mwita amedai kuwa viongozi
mbalimbali hasa wakuu wa mikoa na wkuu wa wilaya wamekuwa wakitumia
madaraka yao vibaya kiasi cha kuingilia majukumu yasiyo yao, na wakati
mwingine kuingilia majukumu ya Bunge, na kutolea mfano Paul Makonda na
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Alexander Mnyeti.
Baada ya hoja yake kukubaliwa na Mwenyekiti wa kikao hicho Mh Andrew Chenge, wabunge wameijadili ambapo wabunge kadhaa akiwemo Ester Bulaya, Zitto Kabwe, Saed Kubenea na Joseph Musukuma wamepata fursa ya kuchangia ambapo kwa kiasi kikubwa wote wameoneshwa kukerwa kauli kauli hiyo inyodaiwa kutolewa na Paul Makonda, pamoja na utaratibu wa wabunge kukamatwa bila utaratibu.
Wakati mbunge Zitto Kabwe akipendekeza
kuitwa mbele ya kamati viongozi waliotuhumiwa, Ester Bulaya amepasua
jipu kwa kusoma ujumbe wa vitisho aliodai umetoka kwa kiongozi mmoja
aliyeteuliwa na Rais.
Akichangia mjadala huo, Waziri
anayehusika na Bunge pamoja na sera Mh. Jenista Mhagama amewataka
wabunge kutomuhusisha Rais Magufuli na makosa yanayofanywa na viongozi
aliowateua ambapo amesema kuwa kwa mujibu wa sheria Rais ana majukumu
yake, na wakuu wa mikoa na wilaya wana wajibu wao, hivyo kama kuna RC au
DC anakwenda kinyume na sheria au kuingilia Bunge, anapaswa
kuwajibishwa mwenye.
Baada ya mjadala huo, Chenge amewahoji
wabunge wanaokubaliana na mapendekezo ya mtoa hoja, ambapo wabunge wote
wameitikia kuunga mkono mapendekezo hayo manne na kuwa maazimio rasmi ya
Bunge
No comments:
Post a Comment