\
Rais wa Jamhuri ya Tanzania John Pombe Magufuli, ameelezea
kusitikishwa kwake na gharama kubwa ya ujenzi wa jengo jipya kwenye
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam.
Gharama hiyo ni ya shilingi bilioni 590, ambayo ni kubwa
ikilinganisha na jengo lililojengwa. Rais Magufuli amesema hayo
alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye uwanja huo.
"Hivi kulikuwa
na sababu gani za nyinyi wataalamu wa serikali kukubali gharama kubwa
namna hii, hivi hili jengo linafanana na bilioni 560," aliuliza Dkt.
Magufuli.
Awali mkandarasi anayejenga uwanja huo ambaye ni kampuni ya BAM
International , alitangaza kusitisha ujenzi huo kutokana na kutolipwa.
Mheshimiwa Rais Magufuli aliahidi kulipa fedha hizo.
Kufuatia hali
hiyo Mheshimiwa Rais mafufuli amemuagiza waziri wa ujenzi, uchukuzi na
mawasiliano Mheshimiwa Prof Makame Mnyaa aliyeongoza nae kuunda timu ya
wataalamu watakaofanya tathimini ya utekelezaji wa mradi huo, ikiwa ni
pamoja na kuzungumza na mkandarasi anayejenga uwanja huo na Mhandisi
mshauri ambao wamekubali kupunguza gharama za ujenzi wa mradi huo
Wednesday, February 8, 2017
Home
Unlabelled
Rais Magufuli asikitishwa na gharama ya ujenzi, uwanja wa ndege
No comments:
Post a Comment