Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony 'Mzee wa Upako' amejitaja kuwa ni mmoja kati ya watu mashuhuri ambao wamewahi kutuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.
Gwajima amefunguka na kusema kuwa yeye
ni mhanga wa suala hilo jambo ambalo lilimpa wakati mgumu sana katika
maisha na kumfanya kunyanyapaliwa na jamii pamoja na watu wake wa karibu
wakiwemo wachungaji wenzake.
Mchungaji Lusekelo amesema hayo
alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachofanyika kupitia ukurasa
wa facebook wa EATV kila Jumatano kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi
jioni.
Lusekelo anadai kuwa mwaka
1997 alituhumiwa kuuza dawa za kulevya lakini anakiri wazi kuwa polisi
wa kipindi kile walikuwa ni wastaraabu kwani waliamuandikia samansi na
kumuomba kufika kituo cha polisi kutoa maelezo, hivyo anasema alifika na
kutoa maelezo yake lakini taarifa hiyo ilivuja mtaani jambo
lililopelekea watu kumtenga.
"Mimi ni mhanga wa dawa za
kulevya mwaka 1997 nilituhumiwa kuwa nauza madawa, lakini wale askari
walikuwa wastaarabu, waliniandikia samasi nikafika kutoa maelezo yangu,
lakini baadaye niliwaambia kuwa wao ni polisi wafanye uchunguzi wao,
walifanya uchunguzi na kugundua mimi sihusiki, watu walifuatilia na
kugundua siyo kweli, na kila mtu akajitoa kwenye, ilionekana kuwa ni
wivu tu, ila mbaya zaidi ile taarifa kuwa niliitwa polisi kwa madawa ya
kulevya ilivuja, hadi wachungaji wenzangu walininyanyapaa, nikivaa suti
au nikiendesha gari kila anajua ni pesa za madawa" alisema Mzee wa
Upako
Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam ambaye kwa takriban wiki moja amekuw akitaja watu mbalimbali
wanaodaiwa kuhusika na dawa za kulevya ambapo katika majina 65 aliyotaja
leo, limo jina la Mchungaji Josephat Gwajima
Mzee wa Upako ameshauri vita ya dawa za
kulevya kwa watu wanaotuhumiwa ni bora viongozi wangetumia njia za
kipolisi kuwataka kufika polisi kwani kutumia njia ya magazeti inaweza
kushusha heshima ya baadhi ya watu ambayo wameijenga kwa miaka mingi.
"Mimi kutokana na tuhuma
zangu kuvuja kuwa niliitwa polisi kwa madawa ya kulevya niliishi miaka
saba watu wananinyayapaa, tena hiyo ni tuhuma tu. Imenichukua miaka saba
kusafisha jina, nimekuja kuanza kusafisha jina mwaka 2005 hivi"
Amesema yeye binafsi anachukia sana dawa
za kulevya kutokana na madhara yake kwa jamii, hivyo hawezi kuthubutu
kujihusisha nazo wala hawezi kuunga mkono watu wanaofanya shughuli hizo
kwa kuwa dawa za kulevya zinaua kizazi cha maendeleo na taifa kwa
ujumla.
Baadhi ya watu katika kipindi hicho
walitaka maoni yake kuhusu Mchungaji Josephat Gwajima kuhusishwa na dawa
za kulevya ambapo Lusekelo alisema hawezi kulizungumzia suala hilo na
kutaka watu wasubiri hadi mwisho wake ufike ndipo na yeye anaweza kusema
lolote
Pia alishauri watu wanaowataja viongozi
waliojijenga kwa muda mrefu kama Mchungaji gwajima wanapaswa kuwa na
uhakika na ushahidi mkubwa usio na shaka, maana ikija kubainika kuwa
siyo kweli, litakuwa ni kazi ngumu kwa viongozi hao kujisafisha kama
ilivyomtokea yeye mwaka 1997.
"Kama kweli kuna wachungaji
wanajihusisha au wanadhaniwa kuhusika kwenye madawa ya kulevya nashauri
tungetumia njia ya wao kuitwa kwa samasi, tunapaswa kuwa makini katika
hili kwani kujenga heshima ni kitu kikubwa, njia ya kuwaita watuhumiwa
kwa njia ya magazeti si jambo nzuri kabisaa" amesisitiza Mzee wa Upako
Kwa wale waliotaka kujua jinsi
anavyomuelewa Mchungaji Gwajima, Lusekelo amesema kuwa Gwajima ni rafiki
yake, na wanaheshimiana sana
No comments:
Post a Comment